Raia katika jimbo la Brandeburg Ujerumani wanapiga kura
22 Septemba 2024Matangazo
Uchaguzi huo unafuatiliwa kwa ukaribu kuona kama chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD kitapata uungwaji mkono mkubwa kwa mara ya pili ndani ya mwezi au ikiwa chama cha Social Democrats SPD kitaibuka kinara.
Brandenburg ndiyo jimbo pekee katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki ambalo limeendelea kutawaliwa na SPD tangu mwaka 1990, kwa kushirikiana na vyama tofauti. Kura za maoni zilizochapishwa na kituo cha ZDF zilionyesha kuwa, AfD ina uwezekano wa kupata kura kwa asilimia 28, huku SDP ikiwa na asilimia 27.
Chama cha Christian Democrats CDU ambacho ni chama kikuu cha upinzani ngazi ya shirikisho, kimepewa asilimia 14 na chama kipya cha muungano wa Sahra Wagenknecht BSW kinasimama katika asilimia 13.