1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Blinken uso kwa uso na Lavrov pembezoni mwa mkutano wa G20

Sylvia Mwehozi
2 Machi 2023

Wanadiplomasia wa Marekani na Urusi wamezungumza kwa ufupi pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka kundi la nchi 20 zilizopiga hatua kiviwanda G20, mkutano ulioshindwa kutoka na tamko la pamoja.

https://p.dw.com/p/4OAl3
Indien Neu Delhi | Bildkombo G20 Außenminister Lawrow und Blinken
Picha: Olivier Douliery/AFP/AP/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wamezungumza kwa ufupi pembezoni mwa mkutano wa wanadiplomasia wa nchi za G20 mjini New Delhi, uliogubikwa na vita vya Ukraine na ambao umeshindwa kufikia tamko la pamoja baada ya pingamizi kutoka Moscow na Beijing.

Indien Neu Delhi | G20 US-Außenminister Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken wakati wa mkutano wa G20 New DelhiPicha: Olivier Douliery/AFP/AP/picture alliance

Blinken amesisitiza dhamira ya Washington ya kumlinda mshirika wake Ukraine ili kuondoa dhana yoyote ya Urusi kwamba Washington inaweza kuyumba katika uungaji wake mkono. Hadi kufikia leo, hapakuwa na mawasiliano ya ana kwa ana baina ya serikali ya Marekani na Urusi tangu Moscow ilipoivamia Ukraine mwaka jana, huku Washington ikisisitiza usaidizi wake kwa Kyiv na kuhimiza juhudi za kimataifa za kuitenga Urusi.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova, aliyelieleza shirika la habari la serikali RIA Novosti, ni kwamba Blinken ndiye aliyeanzisha mazungumzo hayo lakini kwa ufupi sana, baadhi ya ripoti zikisema yalikuwa chini ya dakika 10.

Waziri Lavrov amenukuliwa akisema kwamba kundi la nchi za G20 halitotoa tamko la pamojahuku mwenyeji wa mkutano huo ambayo ni India ikitoa tu muhtasari wa mkutano. Lavrov aliwaambia mawaziri wa mambo ya nje waliokusanyika kuwa wawakilishi wa nchi za Magharibi wamevuruga mkutano huo kwa nia ya kuikosoa Urusi kwa kushindwa kwao wenyewe, na kutoheshimu juhudi za mwenyeji India kufikia makubaliano juu ya masuala mengine. Lavrov anaongeza kwamba.

Indien G20-Treffen in Delhi | Lawrow
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Segei Lavrov akichangia wakati wa mkutano wa G20Picha: Olivier Douliery/REUTERS

"Sisi tumesema hadharani sio mara moja kwamba hatukatai kamwe mapendekezo yanayotolewa kwa nia ya dhati ya kupata suluhisho la kisiasa. Nitakumbusha tena kwamba wakati sisi tunaitwa kwa mazungumzo, sikumbuki kama wenzetu wa nchi za Magharibi, wanaieleza Ukraine ifanye mazungumzo. Pengine, kuna ukweli katika hili, kwasababu Ukraine inatiwa moyo kuendeleza vita."

Majadiliano juu ya tamko la pamoja yameyumba katika masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na msisitizo wa Urusi inayotaka kufanyike uchunguzi wa hujuma ya bomba la kusafirisha gesi la Nord Stream mwaka jana. China iliyo mshirika wa Urusi, nayo imeungana na Moscow katika kuyakosoa mataifa ya magharibi kwa kuanzisha "vitisho" dhidi ya nchi nyingine. Pembezoni ya mkutano huo wa G20 Lavrov amekutana pia na waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang mjini New Delhi na kwa pamoja wamejadiliana juu ya kampeni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine ikiwemo pendekezo la China la kusuluhisha mzozo huo.Mawaziri wa nje wa G20 waombwa kuwa na umoja

Waziri wa mambo ya nje wa India S. Jaishankar naye amesema mkutano huo umeshindwa kufikia tamko la pamoja kwasababu ya tofauti kuhusu vita vya Ukraine.