1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Mazungumzo ya G20 yamalizika bila mwafaka wa Ukraine

2 Machi 2023

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa 20 yalioendelea kiviwanda na yenye uchumi mkubwa zaidi duniani umemalizika Alhamis mjini New Delhi nchini India bila muafaka kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4OAVZ
Indien G20-Treffen in Delhi
Picha: India's Ministry of External Affairs/Handout/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa India Subrahmanyam Jaishankar amesema kulikuwa na "tofauti" kwenye suala la vita vya Ukraine "ambazo hawakuweza kusuluhisha kutokana kwamba kila upande ulikuwa na maoni tofauti.

China na Urusi ndizo nchi pekee wanachama wa G20 ambao hawakukubaliana na uamuzi uliyoitaka Urusi "kujiondoa kikamilifu na bila masharti katika eneo la Ukraine".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na yule wa Urusi Sergei Lavrov walikuwa na mazungumzo mafupi kando ya mkutano huo, ambapo Blinken aliitaka Urusi kubadili uamuzi wake juu ya Mkataba Mpya wa nyuklia.