MigogoroSyria
Marekani yakiri kuwasiliana moja kwa moja na Syria
15 Desemba 2024Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema hayo jana Jumamosi, baada ya mazungumzo kuhusu Syria, wakati akitafuta ushirikiano wa kimataifa katika mchakato wa amani nchini humo.
Blinken amekiri kuwepo kwa mawasiliano hayo ya moja kwa moja, ingawa hakufafanua zaidi na kuongeza kuwa mawasiliano hayo kwa sehemu yalihusiana na kumtafuta Austin Tice, mwandishi wa habari wa Kimarekani aliyetekwa mwaka 2012 baada ya kuanza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Amesema katika mazungumzo na HTS, Marekani "iliwashirikisha kanuni" kuhusu Syria ambazo tayari ameziweka wazi.