SiasaUturuki
Blinken awasili Uturuki kuanza ziara Mashariki ya Kati
6 Januari 2024Matangazo
Blinken atazuru Israel, na mataifa mengine matano ya Kiarabu ya Misri, Jordan, Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, imesema wizara ya mambo ya nje.
Blinken hii leo atafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye ni mmoja ya mkosoaji mkubwa kutoka kwenye ulimwengu wa Kiislamu juu ya namna Marekani inavyoiunga mkono Israel kwenye mzozo huo.
Blinken alitumia ziara za huko nyuma kujaribu kuzuia vita kusambaa, lakini sasa anarejea kwenye ukanda huo ambao umeshuhudia mashambulizi kutokea ama kuelekea Lebanon, Iraq, Yemen, Syria na Iran.