SiasaNigeria
Blinken ainadi Marekani kama mshirika wa usalama Afrika
24 Januari 2024Matangazo
Antony Blinken amelituhumu kundi la Wagner kwa unyonyaji wa mataifa yaliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi au yale yanayoshuhudia mizozo hasa katika ukanda wa Sahel.
Mwanadiplomasia huyo ambaye anaitembelea Nigeria kama sehemu ya ziara yake barani Afrika inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya Washington na bara Afrika, amesema Marekani itaendelea kuisaidia Nigeria na washirika wengine wa kikanda katika juhudi za kuleta utulivu katika eneo la Sahel.
Blinken anafanya ziara katika mataifa manne ya Afrika - Cape Verde, Ivory Coast, Nigeria na Angola - huku akiinadi Marekani kama mshirika muhimu wa usalama kwa Afrika na kudumisha ushawishi wa Washington barani Afrika.