Blinken aendelea na ziara barani Afrika
16 Machi 2023Blinken ni waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa Marekani kufanya ziara Niger, ambacho ni kituo muhimu cha kijeshi cha nchi za Magharibi kinachopambana na magaidi kwenye eneo la Sahel.
Blinken anatarajiwa kutangaza msaada zaidi kwa ajili ya Niger. Awali alipokuwa ziarani nchini Ethiopia, Blinken alieleza kuwa safari zake kwenye nchi hizo mbili ni sehemu ya mpango wa Rais wa Marekani Joe Biden kuwapo barani Afrika pamoja na Waafrika.
Blinken aelekea Niger kuonyesha mshikamano zaidi wa Marekani
Marekani imezindua mpango wa kujihusisha na Afrika kwa kiwango kikubwa kutokana na kuongezeka kwa ushawishi na vitega uchumi vya China katika bara hilo. Blinken alianzia ziara yake nchini Ethiopia, ambapo alikutana na viongozi wa nchi hiyo pamoja na viongozi wa Umoja wa Afrika.