Biden, Scholz kujadiliana msaada kwa Ukraine
9 Februari 2024Mazungumzo ya viongozi hao yanafanyika wakati ambapo mkwamo wa kisiasa katika bunge la Marekani ukizuwia msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine.
Ajenda ya mkutano huo itahusisha pia mzozo katika Kanda ya Mashariki ya Kati, ambako vita vya Israel dhidi ya Hamas vinaendelea.
Soma zaidi: Rais Putin asema hawana maslahi nchini Poland wala Latvia
Katika siku za karibuni, Marekani imefanya mashambulizi dhidi ya makundi yenye silaha yanayohusishwa na Iran, kufuatia mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani.
Soma zaidi: Scholz kuzungumza na Biden juu ya vita vya Ukraine
Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa kijeshi wa Ukraine, ikifuatiwa na Ujerumani, na mkutano wa Biden an Scholz unakuja wakati ikikaribia miaka miwili tangu kuanza kwa vita vya Urusi.