1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz kuzungumza na Biden juu ya vita vya Ukraine

8 Februari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema mazungumzo yake na Rais wa Marekani Joe Biden mjini Washington kesho Ijumaa yatalenga jinsi ya kuimarisha msaada kwa Ukraine ili kuisaidia kupambana na uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4cBfj
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akielekea ziarani nchini Marekani.
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akielekea ziarani nchini Marekani.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Akizungumza katika uwanja wa ndege mjini Berlin muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda Washington, Scholz amesema kile kilichoafikiwa Ulaya na katika Bunge la Marekani hakitoshi kwa sasa kwa hiyo lazima kutafuta njia ya kila mmoja kuongeza msaada wao.

Scholz ataanza ziara yake na hafla ya chakula cha jioni na wabunge kutoka pande zote za kisiasa. Ijumaa asubuhi atakuwa na dhifa ya kifungua kinywa na viongozi wa kibiashara wa Marekani kabla ya kukutana na Biden saa za mchana.

Soma zaidi: Biden and Scholz kujadiliana juu ya msaada mpya kwa Ukraine

Ukraine ambayo inazidiwa katika mbinu na silaha kwenye uwanja wa mapambano katika vita ambavyo vinaelekea mwaka wake wa tatu, inawategemea pakubwa washirika wake wa Magharibi kwa msaada wa kijeshi na kifedha.

Scholz pia atajadili vita vya Israel na Hamas vinavyoendelea kutokota katika Ukanda wa Gaza.