1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden: Mpango wa kuisaidia zaidi Ukraine kutangazwa Alhamisi

26 Septemba 2024

Rais Joe Biden amesema hatua za Marekani kuongeza kasi ya msaada kwa Ukraine zitatangazwa leo Alhamisi, na kwamba wako tayari kuisaidia Kiev kujiimarisha zaidi kuliko hapo awali.

https://p.dw.com/p/4l5FE
Rais wa Marekani JOe Biden (kushoto) akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Marekani JOe Biden (kushoto) akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: BRENDAN SMIALOWSKI/AFP/Getty Images

Duru kutoka kwa maafisa wawili wa Marekani zinaeleza kuwa serikali mjini Washington inatarajia kutangaza msaada wa kijeshi wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 8 kwa Ukraine, utakaojumuisha silaha, droni boti za doria na nyenzo muhimu za uzalishaji silaha.

Soma pia: Zelensky: Umakini wa Marekani utaharakisha mwisho wa vita

Akiwa kwenye mkutano wa kampeni huko North Carolina, rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais Donald Trump amesema Marekani inaendelea kumpatia rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mabilioni ya dola wakati amekataa kuafiki makubaliano ya kumaliza vita na Urusi.