1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Umakini wa Marekani utaharakisha mwisho wa vita

24 Septemba 2024

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema uamuzi makini wa uongozi wa Marekani unaweza kuharakisha hatua ya kukomesha uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi yake kufikia mwakani.

https://p.dw.com/p/4kzyf
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.Picha: Daniel Roland/AFP/Getty Images

Akizungumza mjini Washington baada ya kukutana na ujumbe wa vyama viwili kwenye Bunge la Marekani, Zelensky alisema nchi hizo mbili zina fursa ya pekee ya kuimarisha ushirikiano wao na kuvimaliza vita vya Urusi vilivyoanza tangu Februari 2022.

Rais huyo wa Ukraine yuko ziarani nchini Marekani kukutana na wagombea urais kuwasilisha kile anachokiita "mpango wa ushindi" na pia kuhudhuria mkutano wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa.

Soma zaidi: Urusi yaushambulia mji wa Kharkiv nchini Ukraine na kujeruhi watu 21

Hata hivyo, baada ya mazungumzo yake na Donald Trump, mgombea urais kwa tiketi ya Republican alisema Zelensky anaonekana kama kwamba anataka mgombea urais kwa tiketi ya Democrat ashinde uchaguzi wa Novemba.

Trump alisema endapo atashinda atawataka Rais Vladimir Putin na Zelensky kufikia makubaliano ya kukomesha vita hivyo.