1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden kuongeza muda wa kukaa Marekani kwa wahamiaji wa Sudan

Saleh Mwanamilongo
11 Januari 2025

Utawala wa Rais Joe Biden umesema wahamiaji wapatao milioni moja kutoka El Salvador, Sudan, Ukraine na Venezuela wataruhusiwa kubaki nchini humo kwa miezi 18 zaidi.

https://p.dw.com/p/4p3i6
Biden kuongeza muda wa kukaa Marekani kwa wahamiaji wa Venezuela na Sudan
Biden kuongeza muda wa kukaa Marekani kwa wahamiaji wa Venezuela na SudanPicha: DW

Wahamiaji hao ni pamoja na raia laki sita wa Venezuela na zaidi ya laki moja kutoka Ukraine.

Hatua hiyo imekuja chini ya siku 10 kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump, ambaye ameahidi kuwafukuza wahamiaji haramu.

Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imesema kibali cha kuishi nchini humo kitatolewa kwa raia wa kigeni ambao hawawezi kurudi nyumbani kwa usalama kwa sababu ya vita, majanga ya asili au kwa sababu zingine zisizo za kawaida.