Biden aagiza kufungwa mpaka kati ya nchi yake na Mexico
5 Juni 2024Wakati wa hotuba fupi katika Ikulu ya White House akiwa na maafisa wa majimbo ya mipakani, Rais Joe Biden alisema anafanya kile ambacho wabunge wa chama cha Republican wamekataa kukifanya, akimaanisha kuchukuwa hatua zinazohitajika kulinda mipaka yao. Agizo hilo la Biden linawazuia wahamiaji wanaoingia Marekani kinyume cha sheria kuomba hifadhi katika wakati ambapo idadi hiyo imepita kiasi cha watu 2,500 kwa siku, na pia kurahisisha kurejeshwa kwa watu hao nchini Mexico. Agizo hilo litasalia hadi idadi hiyo itakaposhuka kufikia wahamiaji 1500 wanaovuka kuingia Marekani kwa siku. Wabunge wa Republican wameishtumu hatua hiyo huku makundi ya kutetea haki za binaadamu yakisema yataipinga mahakamani kukomesha sera hiyo kali zaidi ya uhamiaji kuwahi kuptishwa na rais yeyote wa chama cha Democratic kwa miongo kadhaa.