1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden atangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran

Sylvia Mwehozi
16 Septemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden, ameungana na nchi za magharibi kutangaza vikwazo vipya dhidi ya baadhi ya maafisa wa Iran, wakati kukitimia mwaka mmoja baada ya kifo cha msichana Mahsa Amini kilichozusha maandamano makubwa.

https://p.dw.com/p/4WPWn
Großbritannien | Iran Proteste
Picha: Jonathan Brady/PA Wire/empics/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden, ameungana na nchi za magharibi kutangaza vikwazo vipya dhidi ya baadhi ya maafisa wa Iran, wakati kukitimia mwaka mmoja baada ya kifo cha msichana Mahsa Amini kilichozusha maandamano makubwa. 

Biden amesema katika taarifa yake kwamba Wairani pekee ndio watakaoamua hatma ya nchi yao, lakini Marekani itaendelea kushikamana pamoja nao. Naye waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameahidi mshikamano wa Berlin na Wairani katika mkesha wa kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mahsa Amini.Iran yawakamata watu sita wanaotuhumiwa kuandaa ghasia katika maadhimisho ya mwaka mmoja ya kifo cha Mahsa Amin

Vikosi vya usalama vya Iran vimeimarisha doria katika mji wa nyumbani wa msichana huyo ili kudhibiti vurugu zozote zinazoweza kujitokeza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja mwishoni mwa wiki hii.