Watu 6 wakamatwa katika maadhimisho ya kifo cha Mahsa Amin
9 Septemba 2023Kulingana na shirika la habari la Iran IRNA, Shirika la Ujasusi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran IRGS, katika mikoa ya Kohgiluyeh na Boyerahmad limesema limezifungia kurasa tano za mitandao ya kijamii na kuwakamata watu hao wanaotajwa kuziendesha na kusababisha ukosefu wa usalama katika mtandao.
Watu hao wanashukuwa kupanga kufanya vurugu katika siku zijazo
Taarifa ya shirika hilo imeongeza kuwa, sanjari na majaribio ya maadui ya kutaka kusababisha vurugu katika kumbukumbu ya machafuko yaliyotokea mwaka mmoja uliopita, waendeshaji wa kurasa hizo tano walikuwa wakipanga kufanya vurugu katika siku zijazo.
Kifo cha Mahsa Amin kilisababisha maandamano makubwa nchini Iran
Mahsa Amini, aliyekamatwa na polisi mjini Tehran Septemba 13 mwaka jana kwa tuhuma za kuvunja kanuni za mavazi, alifariki dunia Septemba 16 hali iliyosababisha maandamano makubwa kote nchini humo kwa miezi kadhaa. Mamia ya watu walikufa kutokana na maandamano hayo.