1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Dunia yaipa Kenya msaada wa dola bilioni 1.2

31 Mei 2024

Benki ya Dunia imeidhinisha ufadhili wa thamani ya dola bilioni 1.2 kusaidia bajeti ya Kenya ili kuliwezesha taifa hilo la Afrika Mashariki kushughulikia shinikizo la muda mfupi la fedha na kuharakisha sera za mazingira

https://p.dw.com/p/4gTMr
Rais wa Kenya William Ruto akihutubia wakati wa kongamano la COP28 mjini Dubai mnamo Desemba 1, 2023
Rais wa Kenya William RutoPicha: Dominika Zarzycka/NurPhoto/picture alliance

Katika taarifa, benki hiyo imesema ufadhili huo ulikubaliwa huku kukiwa na hali ya kuimarika kwa mazingira ya kiuchumi kufuatia juhudi za serikali za kushughulikia shinikizo la fedha na kushuka kwa imani ya wawekezaji ambavyo vimechangia kushuka kwa thamani ya shilingi.

Benki ya Dunia yasema lengo sasa ni changamoto za muda mrefu

Keith Hansen, mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Kenya, amesema baada ya kushughulikia shinikizo la sasa la fedha, lengo sasa linaelekezwa kushughulikia changamoto za muda mrefu za nchi hiyo.

Masuala yatakayoshughulikiwa na ufadhili wa Benki ya Dunia

Benki hiyo imeongeza kuwa ufadhili huo unalenga kuwezesha ushindani zaidi wa soko la ajira na kuimarisha juhudi za nchi hiyo za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.