1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Dunia yaiidhinishia Nigeria dola bilioni 1.57

30 Septemba 2024

Benki ya Dunia imeidhinisha kitita cha dola bilioni 1.57 kwa Nigeria chini ya mpango mpya wa kuzisaidia sekta kadhaa kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4lENn
Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria.Picha: Nigerian Presidency/Anadolu/picture alliance

Ufadhili huo mpya unajumuisha dola milioni 500 kwa ajili ya kushughulikia masuala ya utawala yanayokwamisha utoaji wa elimu, dola milioni 570 kwa ajili ya utoaji wa huduma za msingi za afya na dola milioni 500 kwa ajili ya mpango wa kuimarisha nishati endelevu na mradi wa kilimo cha umwagiliaji.

Soma zaidi: Nigeria yataka mataifa ya Afrika kupewa kiti cha kudumu Baraza la Usalama

Benki ya Dunia ndiyo taasisi inayoikopesha zaidi Nigeria, ambayo ilipokea mkopo wa zaidi ya dola bilioni 15 mwishoni mwa mwezi Machi, kulingana na data kutoka kwenye Ofisi ya Usimamizi wa Madeni nchini humo.

Benki ya Dunia imesema sehemu ya pesa hizo pia zitatumika kuboresha usalama wa mabwawa ili kuwalinda watu dhidi ya mafuriko.