JamiiUganda
Benki ya Dunia, Ufaransa kuikopesha Uganda dola milioni 600
6 Septemba 2024Matangazo
Taarifa hii imetolewa jana Alhamisi na serikali ya Uganda pamoja na Benki ya Dunia.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, dola milioni 566 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na dola milioni 42.7 zitatolewa na AFD.
Soma pia: Wanaharakati wanaopinga mradi wa mafuta Uganda wakamatwa
Mkopo huo umetolewa wakati raia wa Uganda wakilalamikia usimamizi wa takataka na barabara mbovu za mji mkuu, kutokana na bajeti ndogo kutoka serikalini.
Mwezi uliopita, maporomoko ya takataka yalifukia makaazi ya watu nje kidogo ya mji wa Kampala, na kusababisha vifo vya watu 35.