Bei za mafuta zapanda Tanzania huku nishati hiyo ikiadimika
6 Septemba 2023Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini tanzania (Ewura) imesema kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa asilimia 21 pamoja na hali ya kisiasa katika nchi zinazozalishwa kwa wingi mafuta yaani Opec ndiko kulikosabisha bei ya nishati hiyo kupandishwa nchini.
Kupande bei za mafuta Kenya: Kenya: Mafuta na petroli zapanda bei kwa shilingi 20
Bei hiyo mpya ambayo huenda ikasukuma baadhi ya huduma nyingine kuwa juu, inatofautiana kati ya mkoa mmoja na mwingine, wakati mikoa iliyoko pembezoni mwa nchi kiwango chake ni kikubwa zaidi
Dar es salaam petroli ya lita moja sasa inauzwa kwa shilingi 3,213 ili hali mafuta ya dizeli yakiuzwa kwa shilingi 3,259 bei ambayo utofauti wake ni mdogo na ile iliyoko katika mikoa mingine ya pwani.
Wakati kukushuhudiwa mabadiliko hayo ya bei, hali ya upatikanaji wa huduma hiyo katika baadhi ya maeneo bado ni tete.Saudi Arabia yarefusha muda wa kupunguza uzalishaji mafuta
Licha ya Ewura kusisitiza kuwa akiba ya mafuta inatosheleza, lakini ripoti kutoka sehemu mbalimbali ya nchi zinaonyesha kuwa, watumiaji wa nishati hiyo wanahangaika kutokana na kile kinachoelezwa ni uhaba.
Katika baadhi ya maeneo kumekuwa na ripoti kwamba, wananchi wamelazimika kupanga foleni ndefu kwa ajili ya kupata huduma hiyo na huku kwingine wakiarifiwa kuzozana wakigombea huduma hiyo.
Wananchi wanataka kudhibitiwa kwa hali hiyo kwa kile wanachosisitiza uwezekano wa kuzidisha wasiwasi katika siku za usoni.
Kuhusu kujitokeza kwa hali hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Dr James Mwainyekule aliwaambia waandishi wa habari mwishini mwa wiki kuwa, mamlaka hiyo inawatupia macho wauzaji wa nishati ya mafuta wanaodaiwa kuzidisha hofu kwa wananchi.
Nchi zinazozalisha mafuta ulimwenguni: OPEC+ yapunguza uzalishaji wa mafuta
Alisema tayari vituo viwili vya uuzaji mafuta vilitiwa kufuli ya kutofanya biashara hiyo kwa miezi sita, wakati vingine kadhaa vikiendelea kuchunguzwa.
Duru za habari zinasema baadhi ya wauzaji wa mafuta walijitumbukiza katika mchezo wa kufisha bidhaa, wakiotea ongezeko jipya la bei lilikuwa mbioni kutangazwa kuanzia leo. Bei ya mafuta iliyotangazwa safari hii inaonekana kupanda kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na ongezeko jingine lililotangazwa katika miezi ya hivi karibuni.