1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yarefusha muda wa kupunguza uzalishaji mafuta

5 Septemba 2023

Saudi Arabia imetangaza kurefusha kwa miezi mitatu uamuzi wake wa kupunguza uzalishaji mafuta kwa mapipa milioni 1 kwa siku, ikiwa ni mwendelezo wa shauku yake ya kuona bei ya nishati hiyo inapanda katika soko la dunia.

https://p.dw.com/p/4VzAG
Logo OPEC
Picha: Pavlo Gonchar/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Wizara ya Nishati ya taifa hilo la ghuba imesema uamuzi huo ulianza kutekelezwa mwezi Julai utaendelea hadi mwishoni mwezi Disemba na tathmini ya hali ya soko itafanywa kila mwezi kubaini hatua ziada za kuchukua. 

Saudia ilianza kupunguza kwa hiyari uzalishaji mafuta mwezi Juni mwaka huu baada ya kufikia makubaliano na mataifa mengine ya wazalishaji wakubwa kupitia kundi la OPECna washirika wake ikiwemo Urusi.

OPEC+ yapunguza uzalishaji wa mafuta

Wataalamu wa uchumi wanaamini uamuzi uliotangazwa leo unatokana na Saudia kufadhaishwa na kasi ndogo ya kupanda kwa bei ya mafuta ambayo sasa yanauzwa kwa alau dola 80 kwa pipa kwenye soko la kimataifa.