1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barroso alihutubia Bunge la Ulaya

Kabogo Grace Patricia8 Septemba 2010

Hotuba yake hiyo ililenga zaidi kuhusu uchumi wa Umoja wa Ulaya na kutoa mapendekezo kadhaa kuzuia mizozo mingine ya madeni.

https://p.dw.com/p/P6ZE
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso.Picha: AP

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso amelihutubia bunge la Ulaya kwa mara ya kwanza mjini Strasbourg, akielezea matarajio yake kuhusu uchumi wa umoja huo.

Mwanasiasa huyo wa Ureno, aliwaambia wajumbe wa Bunge la Ulaya kuwa mataifa 27 wanachama wa umoja huo yamekabiliana vizuri na mzozo wa kiuchumi duniani. Hata hivyo, Barroso ameonya kuwa mataifa wanachama yanatakiwa kuungana ili kuufufua uchumi.

Barroso alipendekeza marekebisho kadhaa ili kuzuia mizozo mingine, ikiwemo hatua madhubuti zaidi za kudhibiti soko la fedha na kuanzisha taasisi ya pamoja ya Ulaya kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu.