Baraza la Usalama la UN lataka mjumbe maalum kwa Afghanistan
30 Desemba 2023Hatua hiyo inafuatia ripoti huru ya tathmini iliyotolewa mnamo Novemba ambayo ilitaka ushirikiano zaidi na Afghanistan kufuatia kurejea madarakani kwa Taliban mnamo Agosti 2021.
Azimio hilo linamtaka Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kutaja mjumbe maalum wa kuendeleza mapendekezo ya ripoti hiyo huru, hasa kuhusu masuala ya kijinsia na haki za binadamu.
Azimio hilo lilipitishwa baada ya wanachama 13 wa baraza hilo la usalama kupiga kura ya kuliunga mkono, huku Urusi na China zikikosa kushiriki kura hiyo.
Soma pia:Taliban yaadhimisha miaka miwili tangu kurejea madarakani
Kabla ya kura hiyo, balozi wa Japan katika Umoja wa Mataifa Yamazaki Kazuyuki, alisema kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu na Japan zinaamini kwa dhati kwamba tathmini hiyo huru inatumika kama msingi bora wa mijadala inayofanyika na itakayofanyika.