1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Ukandamizaji wa wanawake unazidi kuongezeka Afghanistan

27 Septemba 2023

Mkuu wa shirika la UN Women, Sima Bahous, ameliomba Baraza la Usalama la Umoja huo kuzisaidia nchi zinazotaka kutangaza kisheria ukandamizaji dhidi ya wanawake na wasichana nchini Afghanistan kuwa ubaguzi wa kijinsia

https://p.dw.com/p/4WsT9
Viongozi wa kundi la Taliban nchini Afghanistan wakimsikiliza waziri mkuu wa utawala wake Mohammad Hasa Akhund wakati wa kongamano la kiuchumi mjini Kabul mnamo Januari 19 2022
Viongozi wa kundi la Taliban nchini AfghanistanPicha: Taliban Prime Minister Media Office/AP Photo/picture alliance

Bahous ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba zaidi ya amri 50 kali za Taliban zinatekelezwa kwa usaidizi kutoka kwa wanafamilia wa kiume. Bahous amesema hali hiyo inazidisha maswala ya afya ya akili na mawazo ya kujiua, hasa miongoni mwa wanawake vijana, na inapunguza maamuzi ya wanawake hata katika nyumba zao wenyewe.

Bahous atoa wito wa msaada zaidi

Bahous ameongeza kuwa wanawake hao wanajiona kama wafungwa waliofungiwa majumbani mwao bila ya matumaini ya siku za usoni. Bahous ameliomba baraza hilo la usalama kutoa msaada kikamilifu kwa mchakato baina ya serikali kuainisha kwa uwazi ubaguzi wa kijinsia katika sheria za kimataifa.

Soma pia:Saluni, maduka ya urembo yafungwa leo Afghanistan

Mkutano huo wa Baraza la Usalama kuhusu ripoti ya hivi karibuni zaidi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu Afghanistan, ulifanyika katika siku ya mwisho ya kongamano hilo la kila mwaka la viongozi wa dunia wa baraza hilo kuu lenye wanachama 193.

Taliban yalikosoa baraza la usalama kwa kuzingatia mambo ya ndani ya Afghanistan

Siku ya Jumatano,  Zabihullah Mujahid, msemaji mkuu wa utawala wa Taliban, alikashifu kikao cha baraza hilo kwa kuzingatia mambo ya ndani ya Afghanistan kama vile elimu ya wanawake na kazi zao badala ya

masuala kama vile usalama, amani na utulivu.

Afghanistan, Kabul | Miaka 2 baada ya Taliban kuingia madarakani, wanawake bado wana haki chache
Wanawake nchini Afghanistan wanaokandamizwa na sheria za utawala wa TalibanPicha: Tolo TV/DW

Soma pia:Taliban kubadili mfumo wa usalama ulioachwa na Marekani?

Katika ujumbe kupitia mtandao wa X ambao awali ulijulikana kama twitter, Mujahid amesema ilikuwa muhimu  kuzungumzia mwisho wa kuondolewa kwa kundin hilo kwenye orodha nyeusi ya Umoja wa Mataifa, kuondolewa kwa vikwazo na kuachiwa kwa mali iliyokamatwa.

Mujahid amesema Umoja wa Mataifa pia ulipaswa kujadili kutambuliwa kwa ufalme wa Kiislamu wa Afghanistan kama vile kundi la Taliban linavyoiita serikali yake.

Utawala wa Taliban bado haujatambuliwa

Hakuna nchi ambayo imeutambua utawala huo wa Taliban na kamati ya stakabadhi za bunge pia haijafanya hivyo, kimsingi kutokana na juhudi zake za kuwadhalilisha wanawake na kuwafanya kuwa tu wa majumbani na kushindwa kuunda serikali jumuishi.

Chini ya sheria za kimataifa, ubaguzi umefafanuliwa kuwa ni mfumo wa ubaguzi wa rangi uliohalalishwa ambao ulianzia Afrika Kusini.

Soma pia:UN yaionya Taliban kuhusu haki za wanawake na wasichana

Lakini makubaliano yanayoongezeka miongoni mwa wataalamu wa kimataifa, viongozi na

wanaharakati yanasema ubaguzi unaweza pia kutumika kwa hali kama zinazoshuhudiwa nchini Afghanistan, ambapo wanawake na wasichana wanakabiliwa na ubaguzi wa kimfumo.