1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock azungumza na Ruto

26 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amefanya mazungumzo na Rais William Ruto wa Kenya Nairobi wakati kukiwa na miito ya kimataifa ya kutaka juhudi zaidi zifanyike kuutatua mzozo nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4bhaJ
Baerbock akiwa Kenya
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, akiwa na Rais William Ruto wa Kenya.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Ofisi ya Rais Ruto imeeleza kuwa, mkutano huo ambao umefanyika katika ikulu ndogo ya Sagana mjini Nyeri, ulijikita zaidi juu ya usalama wa kikanda na mzozo wa nchini Sudan.

Hata kabla ya kuanza ziara hiyo, mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani alikuwa amesisitiza juu ya umuhimu wa kuongezwa juhudi zaidi za kutafuta suluhu juu ya mzozo wa Sudan.

Soma zaidi: Baerbock aiangazia Sudan katika ziara yake ya Afrika Mashariki

Mkutano huo unatokea siku chache tu baada ya maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuutafutia ufumbuzi mzozo kati ya majenerali wawili wanaozozana, mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo nchini Sudan.