1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Baerbock airai Israel kuwalinda raia wa Palestina

8 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya nje Ujerumani ameitolea mwito serikali ya Israel kuchukua jukumu kubwa zaidi la kuwalinda Wapalestina kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi dhidi ya hujuma zinazofanywa na walowezi ya kiyahudi.

https://p.dw.com/p/4azSR
Ramallah | Annalena Baerbock na Riyad Al-Maliki
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock akiwa na mwenzake wa Palestina Riyad Al-MalikiPicha: Anmar Awad/REUTERS

Akizungumza baada ya kukitembelea kijiji kimoja huko Ukingo wa Magharibi, Annalena Baerbock amesema ni wajibu wa serikali ya Israel kusimamia utawala wa sheria pale Wapalestina wanaoishi kihilali kwenye eneo hilo wanaposhambuliwa.

Soma pia: Waliouawa Gaza wapindukia 23,000

Mwito wake unafuatia ripoti za kuongezeka kwa mashambulizi ya walowezi wa kiyahudi dhidi ya Wapalestina tangu wanamgambo wa kundi la Hamas walipoivamia Israel na kufanya mauaji Oktoba 7 mwaka jana.

Baerbock ambaye mapema leo alikuwa mjini Ramallah kwa mazungumzo na viongozi ya Mamlaka ya Wapalestina, amekumbusha kwamba vitendo vinavyoendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi ni kinyume cha sheria za kimataifa.