Bado kuna vizingiti makubaliano ya ukomo wa deni la Marekani
27 Mei 2023Mpatanishi mkuu kutoka chama cha Republican katika makubaliano na serikali ya rais Joe Biden kuhusu kuongeza ukomo wa deni la Marekani amewaambia waandishi wa habari kwamba bado kuna vizingiti vikubwa katika makubaliano hayo.
Makubaliano hayo yanalenga kuongeza ukomo hadi dola trilioni 31.4 ili kuepuka janga linaloweza kusababishwa na serikali kushindwa kulipa deni la taifa.
Wizara ya fedha imesema jana kwamba muda ni mdogo na serikali huenda ikaishiwa fedha ikiwa bunge halitachukua hatua za haraka, ingawa Biden amesema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano.
Soma Zaidi: Wasiwasi waongezeka Washington kabla ya mkutano kuhusu hatma ya madeni ya Marekani
Makubaliano yoyote kati ya rais Biden wa chama cha Democrat na wawakilishi wa Republican yataanzisha mchakato mpya wa kutunga sheria na bunge ambalo hata hivyo limegawanyika, huku wakati wabunge msimamo mkali wa Republican wakitishia kuzuia muswada wowote ambao hautakidhi matakwa yao.