SiasaYemen
Makampuni 18 ya meli yaikimbia njia ya Bahari ya Shamu
4 Januari 2024Matangazo
Mataifa ya Magharibi yanawatuhumu waasi wa Houthi wa Yemen kufanya mashambulizi hayo.
Kulingana na Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya bahari, IMO Arsenio Dominguez jana Jumatano, karibu makampuni 18 ya usafirishaji tayari yameamua kupitia Afrika Kusini ili kuepuka mashambulizi hayo.
Hii inamaanisha kwamba meli hizo zitaongeza siku kumi za safari, hatua itakayoathiri biashara zao na kuongeza gharama za usafirishaji.
Mataifa 12 yakiongozwa na Marekani yamewaonya waasi hao na kuahidi kujibu, ikiwa hawatasisitisha mashambulizi hayo.