1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU walaani mauaji ya watu wengi nchini DR Congo

18 Juni 2024

Umoja wa Afrika walaani mauaji yanayofanywa na waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4hBK6
Moussa Faki Mahamat, Mkuu wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika.
Moussa Faki Mahamat, Mkuu wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika.Picha: Simon Maina/AFP

Umoja wa Afrika siku ya Jumatatu ulitoa taarifa ya kulaani mauaji yaliyotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Juni, ambapo watu 150 waliuawa.

Mkuu wa Halmashauri ya Umoja huo Moussa Faki Mahamat amesema amesikitishwa na ongezeko la mauaji ya raia wasio na hatia yaliyofanywa na vikosi vya Allied Democratic Forces, ADF huko Beni na Lubero, katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Mahamat aidha amezihimiza mamlaka za Kongo kwa kushirikiana na mataifa ya kikanda kuimarisha juhudi zao za kudhibiti kusambaa kwa kitisho cha ugaidi katika eneo zima la Maziwa Makuu.