Athari za vita kwa watoto wanaolindwa na serikali Ukraine
30 Machi 2022Wengi wao walitoka maeneo ambako kuna mapigano na maswali yanayoulizwa ni je nani atajua kama wazazi wao wangali hai, wako wapi au waliuawa?
Kabla Urusi kuivamia Ukraine Februari 24, Ukraine ilikuwa na watoto 100,000 waliowekwa katika takriban vituo 700 vya serikali, shule za bweni au makaazi ya watoto wadogo. Hayo ni kulingana na takwimu za shirika la kuwahudmia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.
Wakimbizi wa Ukraine wapindukia milioni 4
Takwimu za hivi karibuni ambazo shirika la habari la Reuters limepata kutoka wizara ya sera za kijamii, inaonesha tangu vita kuanza, watoto 6,500 miongoni mwa idadi hiyo jumla walihamishwa na kupelekwa maeneo salama nchini humo au nje ya nchi.
Usalama wa watoto watiliwa shaka wakirudi kwa wazazi au walezi
Kulingana na takwimu za hivi karibuni kutoka wizara husika, takriban watoto wengine 47,300 wamerudishwa kwa wazazi au walezi wao, idadi ambayo ni takriban nusu ya idadi jumla ya watoto kwenye mfumo huo. Wataalam wa afya ya akili na wahudumu wa watoto wanasema hatua hiyo huibua changamoto zaidi.
Mzozo wa Urusi na Ukraine watimiza mwezi mmoja
Baaadhi ya watoto hao wanatoka maeneo ambako mapigano yanaendelea. Baadhi yao walioko kwenye mfumo huo, ni mayatima, au walionusuriwa kutoka kwenye familia zilizotumbukia lindi la mihadarati. Isitoshe nusu yao wanakabiliwa na ulemavu au matatizo ya akili.
Vita vinapoendelea, urithi huo wa serikali ya Ukraine tangu nyakati za muungano wa Soviet kuwapa watoto waliokumbwa na changamoto maishani ulinzi na makaazi, sasa unakumbwa na changamoto kubwa zaidi mnamo wakati maelfu kwa maelfu wanayakimbia makwao, hali inayofanya juhudi za kuwapata wazazi wao au jamaa zao kushindikana.
Baadhi ya watoto wanaokimbia vita wajikuta kwenye vituo vya watoto
Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Havryliuk, mmoja wa wahudumu wa watoto ameuliza "sijui hali huwa vipi wakati wa vita. Je wazazi wao watapatikana vipi? Nani anajua ikiwa wangali hai? Na je wenyewe watakuwa vipi ikiwa hali ya hatari imetokea?
Msiwasahau wahamiaji wengine mnapowasaidia wa Ukraine; mashirika
Msichana aliyetambulishwa kwa jina Nina mwenye umri wa miaka 16 alitengana na wazazi wake kwa sababu ya vita mashariki mwa Ukraine, akawasili katika kituo cha watoto cha Lviv.
Mtoto mwengine kwa jina Nastya wa miaka mitano, pamoja na ndugu zake wawili wa miaka saba na tatu, wako katika kituo hicho cha Lviv. Lakini inaonekana hakuna yeyote anayejua nini iliwasibu wazzai wao. Kinachofahamika ni kwamba waliwasili kituoni humo Fabruari 24, siku ambayo uvamizi ulianza.
Serikali yaruhusu watoto kurudishwa kwa wazazi kuwaepusha dhidi ya hatari ya mabomu
Wizara ya sera za kijamii imesema watoto katika vituo 230 waliondolewa, swali la wahudumu wa watoto ni ikiwa wawarudishe kwa wazazi wao au wawapeleke kwingineko salama.
Guterres aitolea mwito Urusi kumaliza vita Ukraine
Mtaalamu wa akili ya watoto Oleksii Heliukh ambaye amekuwa akiwasaidia watoto katika kituo cha Lviv, asema kuwarudisha watoto makwao bila ya uchunguzi muhimu kufanywa, huweza kusababisha madhara zaidi.
Ameeleza kwamba, huwa kuna sababu ya watoto kuondolewa mikononi mwa wazazi wao. Ikiwa sababu hizo hazikushughulikiwa wakati hali ilikuwa tulivu, basi huenda hali ikawa mbaya zaidi wakati wa vita.
Lakini Volodymyr Lys, mkuu wa masuala ya ulinzi wa watoto katika jimbo hilo ametofautiana naye akisema hatari ya vita huwaacha maafisa bila chaguo mbadala.
Kulingana naye, hatari kubwa zaidi ni watoto kuuawa kufuatia mashambulizi ya mabomu. Kwa hivyo haijalishi mzazi ni mbaya au amekosea kiasi gani, bado yeye ni mzazi.
Hali nyingine ya kusikitisha ni watoto wanaokimbilia usalama wakiwa peke yao wasijue wanaelekea wapi.
Mashirika ya misaada ikiwemo Save The Children, yametahadharisha kuwa idadi kubwa ya watoto wamevuka hadi nchi jirani na hata kupita wakiwa peke yao.
Wameelezea wasiwasi wao kwamba ni rahisi kwa watoto kama hao kuwa waathiriwa wa ulanguzi wa wanadamu.
Amanda Brydon, afisa wa ulinzi wa watoto katika Save The Children amesema kinachokosekana ni mfumo wa kuwasajili na kuwafuatilia watoto hao.
(Rtre)