1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assad ameondoka: Je, Syria bado inastahili vikwazo?

8 Januari 2025

Syria ni miongoni mwa mataifa ambayo yamewekewa vikwazo zaidi duniani. Lakini sasa msingi wa mwelekeo wa vikwazo hivyo ambao ulikuwa utawala wa Assad, umeondoka madarakani.

https://p.dw.com/p/4owuK
Wasyria wakishangilia kuangushwa kwa Assad
Wasyria wakishangilia kuangushwa kwa AssadPicha: Benjamin Cremel/AFP/Getty Images

Vikwazo vingi vya kimataifa viliifanya kuwa ni uhalifu kufanya kazi na serikali ya zamani ya Syria. Lakini je, inapaswa kuwa uhalifu kufanya kazi na serikali mpya? Hilo ni swali ambalo mashirika ya misaada, mashirika ya kiraia na wafuasi wa zamani wa Syria wamekuwa wakijiuliza tangu muungano wa makundi ya waasi kuangushwa kwa utawala wa kimabavu wa Assad mwezi uliopita.

Syria kwa muda mrefu imekuwa moja ya nchi zilizowekewa vikwazo zaidi duniani kwa sababu ya familia ya Assad, ambayo iliongoza serikali huko kwa miaka 54. Lakini baada ya kuuondoa utawala huo mapema mwezi Disemba, waasi wa Syria kuunda serikali ya muda, na serikali hiyo ilirithi vikwazo vyote vilivyowekwa kwa serikali iliyopita ya Syria.

Soma: EU kuanzisha mawasiliano na utawala mpya wa Syria

Kwa mujibu wa waziri mpya wa fedha wa serikali ya mpito, Asaad Shaibani alisema vikwazo hivyo vinaizuia Syria kufanya makubaliano ya kuagiza ngano au mafuta kutoka nje. Alikutana na waziri mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, ambaye pia anahudumu kama waziri wa mambo ya nje na kusema nchi yake inaunga mkono "umoja, mamlaka na uhuru wa Syria."

Syria: Wafungwa chini ya utawala wa Assad waachiwa huru

Shaibani pia alitumia ziara yake kuitaka Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Syria, ambavyo vingi iliviweka wakati wa utawala wa Rais aliyeondolewa madarakani Bashar Assad. Waasi wakiongozwa na kundi la Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) walimpindua Assad Desemba 8, kufuatia mashambulizi makali yailodumu katika kipindi kisichozidi majuma mawili.

Soma: Syria baada ya Assad

Tangu wakati huo, mamlaka mpya za Syria imekuwa ikifanya kazi ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na serikali za kikanda na kimataifa, ambazo nyingi zilisitisha uhusiano na Syria kutokana na ukandamizaji mbaya wa Assad dhidi ya waandamanaji.

Baada ya kukutana na Waziri wa Nchi wa Qatar Mohammed bin Abdulaziz Al-Khulaifi, Shaibani alisisitiza wito kwa Marekani kuondoa vikwazo vyake dhidi ya nchi yake. Kituo cha redio cha Syria Sham FM kilimnukuu akisema "Tuliwasilisha kwa Doha wasiwasi wetu kuhusu changamoto zinazohusiana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa kwa watu wa Syria."

Soma kwa kina: Vikosi vya Syria vyaanzisha operesheni Homs

Waziri huyo wa mambo ya nje wa muda alizitaja hatua hizo kuwa ni "kizuizi na kikwazo kwa ahueni ya haraka."  Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa takriban asilimia 90 ya Wasyria wanaishi katika kiwango cha umasikini, na zaidi ya nusu ya watu hawajui hata hatma ya upatikanaji wa mlo wa kawaida.

Kiongozi wa mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa
Kiongozi wa mpito wa Syria Ahmed al-SharaaPicha: Khalil Ashawi/REUTERS

Itakumbukwa Jumalili iliyopita, waziri mpya wa fedha wa Syria, Mohammed Abazeed, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba serikali inapanga kuongeza mishahara ya mwezi ujao kwa wafanyikazi wengi wa sekta ya umma kwa kiwango cha asilimia 400. Ongezeko hilo litafadhiliwa na rasilimali zilizopo za serikali, pamoja na misaada ya kikanda, uwekezaji mpya, na uwezekano wa kufungulia mali za Syria za nje ya taifa hilo.

Soma: Watawala wapya wa Syria wafanya mazungumzo nchini Saudia

Chini ya utawala wa Assad, mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma ilikuwa karibu dola 25 hali iliyokuwa inawafanya wawe chini ya kiwango cha umasikini. Ziara ya Shaibani nchini Qatar, taifa ambalo kwa muda mrefu linaunga mkono upinzani wa Syria ni sehemu ya harakati kubwa zaidi katika eneo hilo.

Ijumaa iliyopita Shaibani kadhalika alikutana na wenzake wa Ujerumani na Ufaransa, Annalena Baerbock na Jean-Noel Barrot, ambao wote walikuwa maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Ulaya kutembelea nchi hiyo ya Kiarabu tangu kuondolewa madarakani kwa Assad.