1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watawala wapya wa Syria wafanya mazungumzo nchini Saudia

Sylvia Mwehozi
3 Januari 2025

Mawaziri katika serikali ya mpito ya Syria wamefanya mazungumzo na maafisa wa Saudi Arabia katika ziara yao ya kwanza ya kigeni tangu kupinduliwa kwa Rais Bashar al-Assad.

https://p.dw.com/p/4omDt
Ujumbe wa Syria nchini Saudia
Waziri wa mpito wa mambo ya kigeni wa Syria Assaad al-Shibani mjini RiyadhPicha: Syrian Foreign Ministry Telegram Channel/AFP

Mawaziri katika serikali ya mpito ya Syriawamefanya mazungumzo na maafisa wa Saudi Arabia katika ziara yao ya kwanza ya kigeni tangu kupinduliwa kwa Rais Bashar al-Assad.

Waziri wa mambo ya kigeni wa mpito wa Syria Assaad al-Shibani amesema kupitia ziara hiyo ya kwanza katika historia ya Syria iliyo huru, wanalenga kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa Syria na Saudia ambao unalingana na historia ya muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

Saudi Arabia ilikata uhusiano na serikali ya Assad mwaka 2012 na kuwaunga mkono waasi wa Syria waliotaka kumpindua katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Lakini mwaka uliopita, Riyadh ilifufua ushirkiano na serikali ya Assad ambao uliirejesha Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.