1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty yaitaka Kongo ichukue hatua za kulinda haki za raia

4 Juni 2024

Mamlaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hazifanyi juhudi za kutosha kuhakikisha viwanda vinalinda haki za binadamu na mazingira katika jamii ambazo watu wanaishi.

https://p.dw.com/p/4gbmq
Haki za Binadamu | Mkurugenzi Mkuu wa Amnesty International Agnes Callamard
Mkurugenzi Mkuu wa Amnesty International Agnes CallamardPicha: Michel Euler/AP/picture alliance

Haya yamesemwa leo na Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu lililo na makao yake mjini London, Amnesty International.

Shirika hilo la haki limeyasema haya baada ya kutazama hali ya kumwagika kwa mafuta na viwanda kutoa moshi.

Amnesty inasema vitendo hivyo vinahusishwa na kampuni ya mafuta ya TotalEnergies EP Congo, Wing Wah na Metssa Congo na athari zake katika pwani ya Atlantic.

Soma pia:Kundi la kutetea haki za binadamu lataka uchunguzi kuhusu 'mauaji' ya baada ya mapinduzi, Kongo

Kampuni ya TotalEnergies EP Congo, iliandikisha angalau umwagikaji wa mafuta mara tatu kutoka mwaka 1972 hadi 2011.

Kampuni hiyo lakini inadaiwa kuchukua hatua ya kusafisha umwagikaji huo wa mafuta.

Ripoti hiyo ya Amnesty lakini pia inasema hakuna uchafuzi wowote uliofanywa kwenye maji, baada ya uchunguzi uliofanywa mwaka 2021.