HRW yataka DRC kuzuwia chuki dhidi ya Watutsi
4 Desemba 2023Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema Luteni Patrick Gisore Kabongo aliuawa katika mji wa mashariki wa Goma mnamo Novemba 9 katika tukio linalodhaniwa kuwa lilichochewa na chuki za kikabila.
Mwanajeshi huyo, aliyekuwa na umri wa miaka 42 na aliyekuwa wa kabila la Tutsi kutoka Kivu Kusini, alishutumiwa na waasi wa M23 kwamba tabia zake zilikuwa tofauti na wao, kulingana na Human Rights Watch.
Soma zaidi: Baraza la Usalama latakiwa kuchukua hatua DRCongo
Kundi la M23 ni kundi la waasi linaloongozwa na Watutsi ambalo limeteka maeneo mengi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu lianze mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021.
Mtafiti mkuu wa shirika hilo la kutetea haki za binadamu, Thomas Fessy, amesema kulaani tu hadharani hakuwezi kuzuia uhalifu huo unaochochewa na chuki katika siku za usoni.