Amnesty: Haki za binadamu duniani zinakabiliwa na vitisho
24 Aprili 2024Katika ripoti yake kila mwaka iliyotolewa leo Jumatano shirika la Amnesty International limeangazia migogoro ya Gaza na Ukraine pamoja na kuenea kwa serikali za kimabavu ambazo zinaharibu utaratibu wa kimataifa kwa kukiuka sheria za kimataifa na kutojali haki za kimsingi.
Katibu Mkuu wa shirika hilo Agnès Callamard amesema kuongezeka kwa migogoro ya silaha, Gaza, Ukraine na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Sudan, Ethiopia na Myanmar akihoji kuwa utaratibu wa kimataifa unaotegemea kanuni uko katika hatari ya kuangamizwa.
Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa lajadili kusitisha mauzo ya silaha kwa Israel
Miongoni mwa mambo mengine, ripoti hiyo inakosoa pia matumizi ya Marekani ya kura yake ya turufu
kulemaza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa miezi kadhaa juu ya azimio la kusitisha mapigano Gaza.