Baraza la Haki za Binaadamu kusitisha silaha kwa Israel?
5 Aprili 2024Matangazo
Iwapo rasimu iliyowasilishwa kwa Baraza hilo siku ya Ijumaa (Aprili 5) itapitishwa, itakuwa ni mara ya kwanza kwa chombo hicho cha Umoja wa Mataifa kuchukuwa msimamo mkali juu ya vita katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa na Israel.
Soma zaidi: Baraza la Usalama lashindwa kupitisha azimio la kusitisha vita Gaza
Rasimu hiyo inatoa wito kwa nchi kusimamisha uuzaji na usambazaji wa silaha na vifaa vingine vya kijeshi kwa Israeli ili kuzuia ukiukaji zaidi wa sheria za kimataifa na ukiukwaji wa haki za binadamu.