Al-Shabaab washambulia kambi ya Umoja wa Afrika, Somalia
27 Mei 2023Shambulizi hilo la wanamgambo wa Al-Shabaab aidha limesababisha kuibuka kwa majibizano ya risasi. Bado haijabainika ikiwa kulikuwa na majeruhi kutokana na mapambano hayo.
Awali, gari lililosheheni mabomu liliendeshwa kuelekea ndani ya kambi hiyo iliyo umbali wa kilometa 120 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu.
Kwa mujibu wa Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika linalojulikana kama ATMIS kambi ya Bulo Marer ilianza kushambuliwa na wanamgambo wa Al shabaab saa kumi na moja asubuhi wakitumia gari hilo lenye vilipuzi na washambuliaji wa kujitoa muhanga.
Akizungumzia shambulio hilo, msemaji wa jeshi la ulinzi la Uganda Felix Kulayigye alithibitisha kutokea kwa shambulio hilo lililowalenga wanajeshi wa Uganda na kuongeza kuwa, jeshi linafanya uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.
Soma Zaidi:Somalia: Al-Shabaab yakamata kambi ya jeshi ya Janay Abdale