1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yatoa wito watu kuchanja

Bryson Bichwa17 Machi 2022

Wataalamu wa afya nchini Afrika Kusini wametoa wito watu ambao hawajachanjwa dhidi ya covid 19 kujitokeza kupata chanjo hiyo ili kuziokoa chanjo laki moja za Pfizer ambazo muda wake wa matumizi unakaribia kumalizika.

https://p.dw.com/p/48dXt
Philippinen | Coronavirus | Symbolbild
Picha: Ezra Acayan/Getty Images

 Afrika Kusini imeorodhesha idadi kubwa ya maambukizi na vifo vya corona katika bara la Afrika, hata hivyo utoaji wa chanjo umesua sua na nchi ina akiba ya dozi milioni 25 za chanjo. Kutoka Pretoria Afrika Kusini, Bryson Bichwa anatuarifu zaidi.

Taarifa ya kumalizika muda wachanjo ya covid 19 ya BioNTech-Pfizer nchini humu imepokelewa kwa maoni mesto.

David Gachupa ni mmoja wa wakazi wa hapa pretoria ambaye anawalaumu baadhi ya raia kuwa chanzo cha chanjo hizo kuishiwa muda wake amesema anashangazwa na baadhi ya watu wanaopuuzia wito wa serikali unaowataka waende kuchanjwa.

Soma zaidi:Hali ya Maambukizi ya corona na ugonjwa wa COVID-19

Alisema inashangaza kuona serikali imepambana na kupata chanjo lakini watu hawataki kuchanja halia ya kuwa tayari kanuni za kupambana na maambukizi mapya zimeanza kulegezwa"cjanjo ilikuwa ni kitu kilichotusaidia sisi kuishi vizuri sana."

Maudhi yasababisha watu kususua chanjo

Watu wengine hususia chanjo hizo kutokana na taarifa wanazopewa na baadhi ya watu walio chanjwa, ya kwamba chanjo hizo zimewasababishia madhara makubwa kiafya.

 Mwanaume mmoja mkazi wa mjini Pritoria ameiambia DW kuwa alipata mabadiliko katika mwili wake wiki mbili tu baada ya kupata chanjo ya Corona"Chamnjo zimeathiri ndoa yangu,sina kabisa hamu ya tendo la ndoa" Alisema huku akiongeza kuwa alimwambia mke wake mambo si kama zamani.

Brasilien | Coronavirus | Impfungen von Kindern
Mvulana akipokea chanjoPicha: Nelson Almeida/AFP/Getty Images

Afrika Kusini imeorodhesha idadi kubwa ya maambukizi na vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 barani Afrika, hata hivyo utoaji wa chanjo umepungua kasi wakati nchi ina akiba ya dozi za chanjo zipatazo milioni 25.

Soma zaidi:Maambukizi ya Omicron Afrika Kusini huenda yamefikia kilele

Profesa Edmond Nyumbu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Eastern Cape nchini Afrika Kusini anaishauri serikali ipanue wigo wake wa kampeni ya utoaji wa chanjo kwa wananchi na kuwaelewesha vya kutosha mchakato ambao chanjo hizo zilipitia kabla ya kuidhinishwa kwa matumizi yake.

Wataalamu:Serikali ifanye kampeni zaidi

 Anaona ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inawaelewesha wananchi kwamba chanjo za Corona hazina madhara kama ambavyo jamii inapokea habari za upotoshaji kutoka kwa baadhi ya watu wachache ambao wamekuwa wakipata maudhi madogomadogo "Chanjo hizi zimefanyika kwa muda mfupi,serikali iwaeleze watu zimepitia mchakato gani na zinatumika kwa m uda gani"

Deutschland, Marburg | Covid-19 Impfstoff-Herstellung bei BioNTech
Wataalamu wakiwa maabaraPicha: Thomas Lohnes/AFP/Getty Images

Serikali imekuwa ikipanga kuweka sheria ya utoaji wa chanjo kuwa ni lazima kama ilivyo kwa jirani yake Botswana lakini hadi sasa hilo limeshindikana hali ambayo imepongezwa na baadhi ya watalaamu wa afya  

Soma zaidi:Mataifa yajipanga kulazimisha chanjo ya corona kwa wote

Huku hayo yakijiri katika saa 24 zilizopita afrika Afrika Kusini watu 1980 wamethibithswa kuambukizwa virusi vya corona na watu watatu wamefariki katika muda huo.

Jumla ya watu 3,698,803 milioni,wameambukizwa virusi vya corona mpaka sasa na jumla ya watu 99,767 wamekufa kutokana na COVID-19.