1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON itaandaliwa kama ilivyoratibiwa

22 Desemba 2021

Mkuu wa shirikisho la kandanda Afrika - CAF Patrice Motsepe amethibitisha kuwa mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika - AFCON itafanyika kama ilivyiratibiwa.

https://p.dw.com/p/44h0U
Fussball - 2021 Africa Cup of Nations - Kamerun
Picha: Alain Guy Suffo/empics/picture alliance

Motsepe amethibitisha kuwa mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika - AFCON yataendelea kama ilivyopangwa nchini Cameroon mwezi ujao licha ya kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19 yanayotokana na kirusi kipya cha Omicron.

Soma CAF kuamua hatima ya mashindano ya Afrika

Motsepe amefuta tetesi kuwa tamasha hilo ambalo liliahirishwa mwaka jana litafutwa tena kutokana na janga la corona.

Tajiri huyo wa madini wa Afrika Kusini Motsepe ameridhia kuandaliwa Afcon baada ya kufanya mazungumzo jana na rais wa Cameroon Paul Biya.

Hata hivyo rais huyo wa CAF mwenye umri wa miaka 59 alisisitiza kuhusu hatari inayojitokeza kutokana na kirusi cha Omicron. Amesema hatua mwafaka zitachukuliwa na hakuna atakayeingia uwanjani bila kuonyesha matokeo ya vipimo vya corona.