1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF kuamua hatima ya mashindano ya Afrika

29 Juni 2020

Maafisa wakuu wa kandanda la Afrika watafanya mkutano wa video kesho Jumanne kujadili hatima ya mashindano kutokana na janga la virusi vya corona, ambalo limesitisha kandanda tangu Machi.

https://p.dw.com/p/3eW5E
FIFA Ahmad Ahmad
Picha: picture-alliance/dpa/Str

Baadhi ya masuala ya kujadiliwa na rais wa Shirikisho la Kandanda Afrika – CAF Ahmad Ahmad ni kamati yake kuu ni pamoja na mashindano ya AFCON yanayohusisha timu 24, yanayotarajiwa kuandaliwa Januari 9 hadi Februari 6 nchini Cameroon.

Na tukibaki huko Afrika ni kuwa jiji la Dar es Salaam limepakwa rangi nyekundu baada ya Simba Sports Club kutawazwa mabingwa wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara. Simba wametwaa uchampioni kwa mara ya tatu mfululizo, lakini pengo la pointi 19 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Yanga, huku ikiwa imebaki na mechi sita mkononi. Watarejea katika mashindano ya Kombe la Mabingwa Afrika ambayo walifika robo fainali katika msimu wa 2018-2019

Wekundi wa Msimbazi pia watakabana koo na Azam FC katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Julai mosi. Washindi wa kombe hilo watafuzu katika Kombe La Shirikisho Afrika.