1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Zoezi la upigaji kura limekamilika Uturuki

14 Mei 2023

Upigaji kura nchini Uturuki umemalizika rasmi na vituo vya kupigia kura vimefungwa jioni hii katika uchaguzi wenye kinyang'anyiro kikali.

https://p.dw.com/p/4RL0M
Türkei | Wahlen 2012 | Auszählung
Picha: Emilie Madi/REUTERS

Upigaji kura nchini Uturuki umemalizika rasmi na vituo vya kupigia kura vimefungwa jioni hii katika uchaguzi wenye kinyang'anyiro kati ya rais aliyepo madarakani, Recep Tayyip Erdogan, na mpinzani wake anayejifungamanisha na mataifa ya Magharibi, Kemal Kilicdaroglu, anayeongoza muungano wa vyama sita vya upinzani.Kwa mujibu wa mamlaka zinazohusika na uchaguzi, idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa kubwa. Uchunguzi wa maoni kabla ya kura hiyo kupigwa ulikuwa unaonesha kuwa wagombea hao wawili huenda wakaibuka na kura zinazokaribiana lakini hakuna kati yao ambaye angelipata kura za kutosha kuunda serikali.Hilo likijiri, kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi, lakini kwa sasa matokeo ya awali yanatazamiwa baadaye jioni ya leo.