Tanzania imeanza zoezi la sensa ya watu na makaazi, zoezi ambalo linafanyika kila baada ya miaka 10 na wananchi wote wamehimizwa kukaa majumbani mwao kusubiri kuhesabiwa. Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan amewarai watanzania wote wajitokeze kwenye zoezi hili muhimu kwa taifa. Zaidi Saumu Mwasimba amezungumza na karani Frank Mawenya akiwa mkoani Simiyu.