1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la kutafuta miili ya maelfu ya Wapalestina linaendelea

20 Januari 2025

Idara ya Huduma za Dharura za Kiraia ya Palestina, yasema shughuli inaendelea ya kutafuta miili ya maelfu ya Wapalestina wanaoaminika kufukiwa chini ya vifusi.

https://p.dw.com/p/4pO1v
Wanajeshi wa Israel wakiondoka kwenye eneo la mpaka katika ukanda wa Gaza mnamo Januari 19, 2025
Wanajeshi wa Israel wakiondoka kwenye eneo la mpaka katika ukanda wa GazaPicha: CTK Photo/ IMAGO

Msemaji wa idara ya Huduma za dharura za Kiraia ya Palestina, Mahmoud Basal, amesema wanatafuta miili ya zaidi ya watu 10,000 wanaoaminika kuwa china ya vifusi na kuongeza kuwa takriban miili 2,840 iliteketea pasi na dalili ya kupatikana kwa mabaki yake.

Usitishaji mapigano unaonekana kudumishwa

Wakaazi na madaktari huko Gaza wanasema kwa sehemu kubwa, usitishaji mapigano unaonekana kudumishwa ijapokuwa kumekuwa na matukio mengine yaliotokea.

Madaktari wanasema watu wanane wamelengwa katika mashambulizi ya Israel tangu leo asunuhi katika mji wa kusini wa Rafah bila ya kutoa maelezo zaidi.

Malori ya misaada yaanza kuingia Gaza

Nchini Israel pia hali ya mashaka inaendelea kuhusu mateka waliosalia Gaza iwapo wataweza kuokolewa katika kipindi kirefu kwa utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha vita.

Ndugu wa mmoja wa mateka waGazaAshley Waxman Bakshi, amesema wanataka kuhakikisha kuwa mwendelezo wa majadiliano ya awamu ya pili unatokea, na kuonya kuwa mambo bado.

Malori 220 ya misaada yatumwa Gaza

Takriban malori 220 ya misaada yalitumwa kutoka Misri kuelekea Ukanda wa Gaza hii leo.

Afisa wa shirika la Hilali Nyekundu wa Misri huko Sinai Kaskazini, amesema lori hizo ni pamoja na 10 za kubeba mafuta na kwamba zitaingia Gaza kupitia kivuko cha mpakani cha Keremu katika eneo la kusini.

Malori ya msaada wa kiutu katika kituo cha ukaguzi cha Baloza kuelekea Rafah kati ya Misri na Ukanda wa Gaza Jumapili Januari 19, 2025
Malori ya msaada wa kiutu katika kituo cha ukaguzi cha Baloza kuelekea RafahPicha: Amr Nabil/AP Photo/picture alliance

Afisa huyo amoengeza kuwa kuna malori 3000 yaliobeba msaada wa kiutu tayari kupelekwa katika ukanda wa Gaza.

Kulingana na mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu, Tom

Fletcher, zaidi ya malori 630 yenye misaada ya kibinadamu yaliingia Gaza na angalau 300 kati yao yanapelekwa sehemu ya kaskazini ya eneo hilo la Gaza.

Vikwazo vyaondolewa dhidi ya meli zinazohusishwa na Israel

Kituo cha Kuratibu Shughuli za Kibinadamu HOOC chenye makao yake mjini Sanaa ambacho pia ni kiungo cha mawasiliano kati ya vikosi vya Kihouthi na wahudumu wa meli za kibiashara kinachohusishwa na tawi la kijeshi la Houthi, kimesema kinasitisha vikwazo dhidi ya meli zinazomilikiwa na watu binafsi au mashirika ya Marekani au Uingereza, pamoja na meli zinazosafiri chini ya bendera zao.

Usitishaji mapigano waanza kutekelezwa Gaza

Katika barua pepe iliyotumwa kwa maafisa wa sekta ya usafiri wa meli mnamo Januari 19, kituo hicho kimesema kinathibitisha kwamba katika tukio la uchokozi wowote dhidi ya Yemen kutoka kwa Marekani, Uingereza au Israeli, vikwazo hivyo vitarejeshwa dhidi ya mataifa hayo.