JamiiZimbabwe
Zimbabwe yawaachia wafungwa kupunguza msongamano magerezani
20 Mei 2023Matangazo
Karibu wafungwa 800 waliachiliwa huru Ijumaa, kutoka katika gereza kuu na lile la Chikurubi kwenye mji mkuu, Harare.
Kwa mujibu wa msemaji wa huduma za magereza na urekebishaji tabia nchini Zimbabwe, Meya Khanyezi, magereza katika sehemu mbalimbali nchini humo yalianza kuwaachilia wafungwa waliofuzu kupata msamaha wa Rais tangu Alhamisi.
Jela za taifa hilo zina uwezo wa kuhifadhi wafungwa 17,000 lakini kwa sasa, zina zaidi ya wafungwa 20,000.