1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Zimbabwe yatangaza Agosti 23 kuwa tarehe ya uchaguzi mkuu

1 Juni 2023

Zimbabwe imemaliza utata wa miezi kadhaa juu ya tarehe ya uchaguzi wa rais, unaotarajiwa kuwa mpambano mpya baina ya rais wa sasa Emmerson Mnangagwa na mgombea wa upinzani, Nelson Chamisa.

https://p.dw.com/p/4S4Ip
Simbabwe | Wahllokal in Harare
Picha: Tsvangirayi Mukwazhi/AP Photo/picture alliance

Gazeti rasmi la serikali limethibitisha kuwa uchaguzi wa rais, ule wa wabunge na wa serikali za mitaa utafanyika tarehe 23 Agosti.

Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80 alichukua madaraka mwaka 2017 kupitia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya mtangulizi wake Robert Mugabe, na anaongoza chama cha ZANU-PF kilichopo madarakani tangu Zimbabwe ilipopata uhuru mwaka 1980.

Soma pia: Rais wa Zimbabwe Mnangagwa aahidi uchaguzi wa "huru na haki"

Mpinzani wake mkuu, Nelson Chamisa mwenye umri wa miaka 45, ambaye ni mwa mwanasheria na mhubiri, anaongoza chama kipya cha Citizens Coalition for Change, CCC na alishindwa na Mnangagwa kwa kura chache katika uchaguzi wa 2018.

Wachambuzi wanatarajia ushindani mkali katika taifa hilo la kusini mwa Afrika linalokabiliwa na changamoto lukuki za kiuchumi.