1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiZimbabwe

Zimbabwe yapongezwa kwa kuondoa adhabu ya kifo

3 Januari 2025

Umoja wa Mataifa umeipongeza Zimbabwe kwa kuondoa hukumu ya kifo, na kuzitaka nchi nyingine kuchukua hatua sawa na hiyo, au angalau kusitisha kwa muda adhabu ya kifo.

https://p.dw.com/p/4omyL
DW Explainers "Internationaler Tag gegen Todestrafe"

Siku ya Jumanne, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alisaini sheria ya kuondoa adhabu ya kifo, hatua itakayobatilisha adhabu hiyo kwa wafungwa wapatao 60 ambao walihukumiwa kunyongwa.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa,Volker Turk, amesema anaipongeza hatua ya Rais Mnangagwa kuondoa rasmi adhabu ya kifo.

Sheria ya Kukomesha Adhabu ya Kifo nchini Zimbabwe inaeleza kuwa sasa mahakama haziwezi tena kutoa hukumu ya kifo, na hukumu zozote za kifo zilizopo lazima zibadilishwe na kuwa kifungo gerezani.

Hata hivyo, kipengele kimoja kinasema hatua ya kukomeshwa kwa hukumu ya kifo inaweza kuondolewa wakati wa hali ya hatari.