1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky: Vita vya Bahari Nyeusi vitaingia katika historia

1 Novemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema vikosi vyake vitafanikiwa siku zijazo katika vita vyake dhidi ya Urusi haswa katika eneo la Bahari Nyeusi.

https://p.dw.com/p/4YGfG
Ukraine Präsident Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: president.gov.ua

Zelensky amesema ushindi huo utazingatiwa hapo baadaye katika historia licha ya kuwa kwa sasa hali ni ngumu katika uwanja wa mapambano.

Akilihutubia taifa hapo jana katika ujumbe wake wa video, Zelensky ameonya kuwa ulimwengu wa sasa umeundwa katika mazoea ya kupata mafanikio haraka na kusema Urusi ilipoanzisha uvamizi wakeFebruari mwaka jana, watu wengi duniani hawakutarajia kuwa Ukraine ingehimili na kujizatiti.

Soma pia: Urusi imeivamia Ukraine kwa miaka miwili na zaidi na imeendeleza mashambulizi nchini humo.

Mapigano makali yanaendelea hasa eneo la mashariki karibu na mji wa Avdiivka. Kyiv kwa sasa inajaribu kuyakomboa maeneo yote yanayokaliwa kimabavu na Moscow, ikiwa ni pamoja na rasi ya Crimea katika Bahari Nyeusi ambayo ilinyakuliwa kinyume cha sheria na Urusi mnamo mwaka 2014.