SiasaUkraine
Zelensky kwenda Uswisi kuimarisha uungaji mkono wa kimataifa
15 Januari 2024Matangazo
Tangazo la ziara hiyo limetolewa na ofisi ya kiongozi huyo usiku wa kuamkia leo.
Akiwa nchini Uswisi Zelensky atakutana na viongozi wakuu wa mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na rais wa Uswisi na kisha kuhudhuruia Kongamano la Uchumi duniani linalofunguliwa leo huko kwenye mji wa Davos.
Ziara hiyo ilitangazwa saa chache baada ya Ufaransa na Ujerumani kusisitiza azma yao ya kuendelea kuiunga mkono Ukraina katika vita dhidi ya Urusi.
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi hizo mbili, wamesema kwa nyakati tofauti kuwa watakuwa pamoja na Ukraine kwa muda mrefu kadri itakavyohitajika.