1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky atoa wito wa mshikamano baada ya shambulio la Urusi

17 Aprili 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amewatolea wito washirika wake wa Magharibi kuwa na nia thabiti na kutoa msaada wa kutosha baada ya mashambulizi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4esO5
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymir ZelenskyPicha: Gints Ivuskans/AFP

Zelesky ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram na kusisitiza kuwa hilo lisingelitokea kama Ukraine ingepokea vifaa vya kutosha vya ulinzi wa anga na ikiwa ulimwengu ungekuwa na ari ya kukabiliana vilivyo na ugaidi wa Urusi.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la nchi saba tajiri zaidi duniani wanakutana katika kisiwa cha mapumziko cha Italia cha Capri, ili kujadili mizozo inayoendelea ikiwa ni pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na na mvutano unaoongezeka katika kanda ya Mashariki ya Kati.