Zelensky atoa wito kwa utengenezaji wa droni Ukraine
9 Januari 2025Matangazo
Rais Zelensky ametoa mwito huo katika mkutano wa kundi la mataifa linaloiunga mkono Ukraine uliofanyika leo katika kambi ya jeshi la Marekani ya Ramstein nchini Ujerumani.
Zelensky amesema matumizi ya droni yamebadilisha jinsi vita vinavyopiganwa, na kwamba kuwezeshwa kwa Ukraine katika nyanja hiyo kumeisaidia kuzuia mashambulizi ya Urusi.
Kiongozi huyo pia ameliomba kundi hilo lenye takriban nchi 50 kuipa silaha zaidi za kuzuia mashambulizi ya anga hasa baada ya Urusi hivi karibuni kufanya mashambulizi mabaya ya anga kaika mji wa Zaporizhzhya yaliyosababisha vifo vya watu 13.
Amewataka pia washirika wake kuiwekea vikwazo vikali zaidi sekta ya nishati ya Urusi ili kupunguza mapato ya Moscow.