Zelensky amteuwa kamanda mpya wa vikosi vya ardhini
11 Februari 2024Pavliuk, luteni jenerali aliyehudumu katika wadhifa huo wa wizara kwa muda wa mwaka mmoja, anachukua nafasi ya kanali jenerali Oleksandr Syrskyi baada ya kutimuliwa kwake kuongoza jeshi la Ukraine.
Zelensky atangaza uteuzi wa nyadhifa nyingine za kijeshi
Hapo jana Jumamosi, Rais Zelenskiy alitangaza uteuzi wa nyadhifa nyingine tano za kijeshi, na kujaza kikosi kinachojiimarisha tena kiulinzi dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini humo ambao sasa umedumu kwa takriban miaka miwili.
Soma pia:Urusi yaishambulia tena Kyiv kwa makombora
Ukraine inakabiliwa na uhaba wa wapiganaji na vifaa inapoingia mwaka huu wa 2024 baada ya kupata mafanikio machache katika uwanja wa mapigano mwaka uliopita.
Pia inakabiliwa na hali ngumu kwa kutopokea misaada ya kijeshi kutokaMarekaniambayo ndiyo muungaji wake mkono mkubwa